Michezo
Jay Z na Beyonce waisaidia Cleveland Cavaliers kuifunga Golden State Warrior
Beyonce alisitisha ziara yake ‘Formation Tour’ na kuhudhuria kwenye mchezo kikapu wa sita kati ya Golden State Warrior dhidi ya Cleveland Cavaliers akiwa na mumewe, Jay Z.
Mastaa hao walikuwa kivutio kikubwa kwenye mchezo huo ambao walionekana kuitia nguvu kwa kuonyesha ushirikiano kwa timu yao hiyo ya Cleveland Cavaliers ambayo iliibuka na ushindi wa vikapu 115 dhidi ya vikapu 101 vya Golden State Warrior.
Mpaka sasa timu hizo zinasubiria mchezo wa mwisho [saba] ambao utachezwa kwenye uwanja wa Cleveland Cavaliers ndiyo utaamua nani mshindi kutokana na timu hizo kila moja imeshinda mechi tatu kwenye michezo sita iliyopita.
Taza video hapa.
https://youtu.be/9Bz1KvhUcLs