Kiungo wa Yanga Pacome Zouzoua amefanikiwa kujumuishwa kwenye kikosi cha Taifa lake Ivory Coast kwa mara ya kwanza.
Pacome amejumuishwa kwenye kikosi hicho kinachojulikana kama Tembo kinachoenda kushiriki Fainali za Mataifa ya Afrika yatakayofanyika nchini Ivory Coast, ingawa amewahi kuizitumikia timu za Taifa kwa vijana lakini haikuwa rahisi kuitwa timu ya wakubwa.