Miamba ya soka Afrika Mashariki na Kati, Simba SC imemtambulisha rasmi Mshambuliaji wa JKU ya Zanzibar, Saleh Karabaka maarufu kama Tumbo Jr kuwa mchezaji wao.
Usajili wa Karabaka mwenye umri wa miaka 23 unakuwa wa kwanza katika dirisha hili dogo.
Karabaka tayari amejiunga na timu Visiwani Zanzibar na ataanza kuonekana akiwa na jezi ya Mnyama katika michuano ya Mapinduzi inayoendelea.