Burudani
Nicki Minaj kutua Bongo?!
Yasemekana kwamba msanii wa kike wa Hip Hop kutoka nchini Marekani Nicki Minaj anatarajiwa kuja nchini Tanzania kupiga shoo mwezi wa kwanza Mwakani.
Kwa habari zisizo na uhakika zilizofikia B5, msanii Nicki Minaj anatarajiwa kutua Bongo kupiga shoo katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam pamoja na wasanii wengine ambao watatangazwa baadae.
Inasemekana shoo hiyo itakuwa ikihusiana na shughuli ya mpira wa miguu ambapo timu kadhaa za ulaya, ujerumani na ufaransa zinatarajiwa kuja Tanzania kwa ajili ya uzinduzi rasmi wa timu ya African Lyon.