Habari

TAWLA: Wanawake 400,000 nchini hutoa mimba kwa siri kila mwaka

Mikoa ya Mwanza na Dar es salaam inatajwa kukabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa huduma za afya ya uzazi na vifo vitokanavyo na utoaji mimba usio salama, hali inayosababisha wanawake zaidi ya 400,000 kulazimika kutoa mimba kwa usiri mkubwa kila mwaka huku asilimia 40 kati yao wakiishia kupata matatizo makubwa ya kiafya.

Akiwasilisha tathimini ya utekelezaji wa maazimio na mpango kazi wa shughuli za chama cha wanawake wanasheria tanzania ( TAWLA ) kwa mwaka 2016 juu ya umuhimu wa afya ya uzazi,Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la kivulini mwanza Yassin Ally amesema asilimia 60 ya wanawake hapa nchini wenye matatizo ya utoaji mimba hawapati kabisa huduma ya matibabu wanayoyahitaji.

Marina Mashimba ni wakili wa kujitegemea jijini Mwanza,anasema ili kupunguza au kuondoa kabisa vifo vya akinamama na wasichana vitokanavyo na utoaji mimba usio salama,TAWLA imejikita katika kupigania haki za wanawake na usawa wa kijinsia hapa nchini ikiwemo haki ya afya ya uzazi katika kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii pamoja na kuondoa imani potofu kuhusu afya ya uzazi.

Mwaka 2007 Tanzania iliridhia mkataba wa nyongeza wa haki za wanawake afrika ( Maputo Protocol ) wa mwaka 2003,ambapo katika ibara ya 14 ( 2 ) ( c ), unatamka kuwa nchi wanachama zitachukua hatua madhubuti kulinda haki za uzazi za wanawake kwa kuruhusu utoaji wa mimba pale ambapo mimba imepatikana kwa ukatili wa kijinsia kubakwa,kufanya ngono maharimu au kama kuendelea kukua kwa mimba hiyo kunahatarisha hali ya mama ya kiafya na kiakili na mtoto aliye tumboni.

Source: ITV

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents