Burudani

Afande Sele asema amechoka maisha ya ukapera

Baada ya hivi karibuni rapper kutokea Morogoro, Afande Sele kudai kuwa hana mpango wa kufunga ndoa, Jumatano hii ametengua kauli hiyo kwa kudai kuwa amechoka maisha ya ukapera.
Afande Sele akiwa na watoto wake Mkubwa anaitwa Tunda na mdogo Sanaa
Afande Sele akiwa na watoto wake mkubwa anaitwa Tunda na mdogo Sanaa

Rapper huyo ambaye kwa sasa ana jukumu la kuwalewa watoto wake wawili ambao mama yao alishafariki dunia, ameonyesha kuchoshwa na kazi mbalimbali za nyumbani ambazo analazimika kuzifanya.

“Najisikia kuoa tena,” alisema Afande. “Mara chache huamua kula kwenye sufuria kwa sababu naishi mwenyewe hivyo napika mwenyewe, naosha vyombo mwenyewe nk, hivyo kwasababu ya uvivu wangu katika kuosha vyombo wakati flani huamua kula kwenye sufuria ili kuepuka kuchafua vyombo zaid pasi na ulazima,” aliandika kupitia facebook yake.

Hivi karibuni alikaririwa na chombo kimoja cha habari akidai kwa sasa yupo kwenye mchakato wa kumtafuta mwanamke sahihi ambaye atafanya naye maisha.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents