Burudani

Agnes Masogange adai sababu iliyomfanya Tekno amkane ni ukaribu wake na Davido!

Mrembo Agnes Masogange ameendeleza episode nyingine ya drama yake na mwimbaji wa Nigeria, Tekno miles, iliyoibuka wiki hii baada ya mwimbaji huyo kukanusha kuwa hajawahi kuvunja naye amri ya sita!

maso

Katika muendelezo wa kutaka kuthibitisha kuwa alichokisema Tekno sio kweli, Agnes ameweka wazi sababu anayodai kuwa ndiyo iliyomfanya mwimbaji huyo wa ‘Duro’ amkane, kuwa ni wivu baada ya kuona amekuwa karibu na super star mwingine wa Naija, Davido.

Agnes na Davido

Agnes alipost picha aliyowahi kupost miezi kadhaa iliyopita akiwa anakula bata na Davido na kuandika caption, “Kumbe brother alipanick kitambo kisa OBO Baddest”, post ambayo baadae aliifuta.

Hii ni video inayowaonesha Masogange na Davido wakishare kinywaji walipokuwa wakila bata.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents