Michezo

Ahsanteni Tanzania kwa ukarimu wenu – Mamelodi Sundowns

Maimba ya soka nchini Afrika Kusini, Mamelodi Sundowns Football Club wamewashukuru Watanzania kwa ukarimu wao katika kipindi walichokuwa hapa nchini wakijiandaa na mchezo wao wa klabu bingwa Afrika.

Mamelodi wamefanikiwa kuwafunga CR Belouizdad magoli 5 – 1 ambao ndiyo waliyokuwa wenyeji baada ya Waalgeria hao kuuomba Uongozi wa Shirikisho la Mpira nchini Tanzania TFF kuutumia uwanja wa Mkapa kama dimba lao la nyumbani hapo jana.

”Tunaondoka na magoli matano na pointi 3 lakini mioyo yetu inabakia Tanzania! 🇹🇿. Ahsanteni sana kwa ukarimu wenu!,” wameandika Mamelodi Sundowns.

Magoli ya Sundowns yalifungwa na (5′, 55′ Zwane, 48′ Shalulile, 75′ Maboe, 89′ Erasmus) wakati lile la wenyeji CR Belouizdad likifungwa na (44′ Sayoud).

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents