Habari

Ajinyonga kwa kushindwa kurejesha mkopo

Mkazi mmoja wa mtaa wa Tambukareli, Manispaa ya Shinyanga, Sarah Bundala (55) amekutwa amejinyonga chumbani kwake baada ya kushindwa kufanya marejesho ya mkopo aliokuwa amemdhamini rafiki yake aliyetoroka na pesa, ingawa haijafahamika ni kiasi gani.

Tokeo la picha la
Kamanda, Jumanne Muliro

Akithibitisha taarifa hizo Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga, Jumanne Muliro amesema tukio hilo limetokea juzi (Ijumaa Tar 14 Julai) majira ya saa 10:00 jioni.

Kamanda Muliro amesema kabla ya kujinyonga, mama huyo alikuwa na rafiki yake wakihangaika pamoja kutafuta pesa ili apate za kupeleka kwenye marejesho ya mkopo ambao alikuwa amemdhamini rafiki yake aliyetoroka kusikojulikana.

Akielezea tukio hilo, rafiki wa karibu na marehemu, Mariamu Mugaya amesema majira ya saa 8:00 mchana alimwita ili amsindikize kutafuta pesa za kurudisha mkopo, lakini walizunguka bila mafanikio, ndipo akamshauri ampigie simu mumewe amsaidie kiasi hicho cha pesa anachohitaji, lakini akagoma kufanya hivyo.

Baada ya kushauriana mahala pa kupata pesa, lakini wakazikosa, marehemu alimwambia aenda nyumbani, ili yeye akalale kwanza na ikifika majira ya saa 10:00 jioni arudi kumuona na kwamba hata watu wakimuuliza yuko wapi, awaambie amelala nyumbani kwake asiwafiche. Lakini ilipofika muda huo, akapokea taarifa ya kujinyonga kwa rafiki yake.

Chanzo : HabariLeo

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents