Habari

Mbunge apigwa na ‘mayai viza’ katikati ya harusi (+Video)

Mbunge wa jimbo la  Parana huko nchini Brazil, Maria Victoria Barros (25) amejikuta akipigwa na mayai viza katikati ya harusi yake na waandamanaji wa Chama cha Mrengo wa kushoto kinachompinga Rais wa Brazil, Michel Temer.

Bi Maria Victoria Barros na Mmewe

Mamia ya waandamanaji walikusanyika nje ya kanisa  ambapo sherehe za harusi zilifanyika Ijumaa ya wiki hii (Tar 14 Julai) jioni huku wengi wakimkashifu Mbunge huyo na Baba yake mzazi, Ricardo Barros ambaye ni Waziri wa michezo kuwa waliunga mkono sera ya kupigwa marufuku kwa wageni kipindi cha uchaguzi na kumuunga mkono Rais Temer .

Baba Mzazi wa Mbunge huyo, Ricardo Barros ni moja ya Watu waliohudhuria kwenye sherehe hiyo ambayo iliingiwa na dosari ya vurugu.

Kwa ushahidi wa video zinazoonekana kupitia mtandao wa Youtube zinaonesha Mbunge huyo akitoka Kanisani na ulinzi mkubwa huku akikingwa na mwavuli kuzuia mayai yasimpige.

 

Mzee Ricardo Barros ni moja ya Viongozi wa mbele ambao walimpigia kampeni Rais wa sasa wa Brazil, Michel Temer na tayari ameteuliwa kuwa Waziri wa Afya wa Brazil.

Hata hivyo kwa kile ambacho waandamanaji hao walionekana wakiimba ni Rushwa na ulafi wa madaraka ambapo familia nzima ya Mzee Barros wote ni viongozi wakubwa Serikalini.

Tazama video ya tukio hilo hapa chini.

https://youtu.be/Syp1YPTIJ9M

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents