Burudani

Album ya ‘Invasion of Privacy’ ya Cardi B yagonga Gold kwenye mauzo

Ikiwa ni siku sita tu zimepita tangu rapa Cardi B aachie album yake ya kwanza ya ‘Invasion of Privacy’ tayari album hiyo imeshagonga Gold kwenye mauzo yake sokoni.

Kwa maanahiyo album hiyo ndani ya siku sita tayari imeuza nakala (Copy) zaidi ya laki tano sokoni huku nyimbo za album hiyo ikiwemo wa Be Careful ukishika nafasi za juu kwenye chati za Billboard.

Kutokana na hatua hiyo tayari chama cha Recording Industry Association of America (RIAA) kimempongeza na kumkabidhi cheti rapa huyo.

Album ya Invasion of Privacy ina nyimbo 13 na tayari mastaa kama Drake, Lil Wayne, Miss Eliott, Oprah na wengine wengi wamempongeza rapa huyo wa kike aliyekuja kwa kasi zaidi kwenye game ya muziki wa Hip Hop nchini Marekani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents