Habari

Alichokizungumza Makamu wa Rais siku ya mazingira duniani

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan amewataka Viongozi wa ngazi zote kuongeza nguvu katika utekelezaji wa Sera, Sheria, Mikakati na miongozo katika kukabiliana na uharibifu wa mazingira.

Makamu wa Rais wa ameyasema hayo wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambayo kitaifa yamefanyika jijini Dar es Salaam kwenye Viwanja vya Mnazi mmoja.

“Ni muhimu, mipango ya maendeleo katika kukabiliana na uharibifu wa mazingira ili nchi yetu iwe na maendeleo endelevu” alisema Makamu wa Rais.

Makamu wa Rais amesema kazi ya kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa hifadhi ya mazingira unahitaji ushirikiano wa wadau wote kwa ngazi zote.

Maadhimisho ya Kimataifa yanafanyika India katika mji wa New Delhi yakibeba ujumbe wa kuhimiza kupunguza uchafuzi wa mazingira kutokana na matumizi ya bidhaa za plastiki (Beat Plastic Pollution) lakini hapa nchini Kitaifa ujumbe wa maadhimisho ni “Mkaa Gharama: Tumia Nishati Mbadala”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents