Michezo

VIDEO: Singida United wafuata nyayo za Simba, watinga nusu fainali michuano ya SportPesa Super Cup

Klabu ya Singida United imeungana na Simba kuingia hatua ya nusu fainali ya mashindano ya SportPesa Super Cup kwa ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya AFC Leopards kwa changamoto ya mikwaju ya penati baada ya timu hizo kutoka sare ya 0-0 ndani ya dakika 90.

https://youtu.be/zkxYOjwS_ws

Mlinda mlango wa Singida United, Manyika Junior ameibuka na tuzo ya Man Of The Match baada ya kuokoa penati zilizowapa ushindi vijana hao wa Singida.

Kwa matokeo hayo, Singida United inakuwa klabu ya pili kutoka Tanzania kufuzu nusu fainali baada ya Simba kufanya hivyo jana huku klabu ya Yanga na JKU zote kutoka Tanzania zikitolewa mapema kwenye michuano hiyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents