Habari

Aliyepindua nchi ajiuzulu na kukimbia

Kiongozi wa kijeshi nchini Burkina Faso, Paul-Henri Sandaogo Damiba amekubali kujiuzulu jana, siku mbili baada ya maafisa wa kijeshi kutangaza kwamba wamemuondoa madarakani.

Viongozi wa kidini wamesema kuwa Luteni Kanali Damiba ameomba kujiuzulu ili kuepusha madhara yanayoweza kusababishwa na makabiliano.

Hatua hiyo inatokana na mazungumzo yaliyofanyika kati ya Damiba na kiongozi mpya aliyejitangazia madaraka, Kapteni Ibrahim Traore. Viongozi wa kidini waliosaidia katika juhudi za upatanishi wamesema Damiba ametoa masharti saba ili aweze kuondoka madarakani, ikiwemo kuhakikishiwa usalama na haki yake pamoja na usalama wa washirika wake katika jeshi.

Pia amewataka waliochukua madaraka kuheshimu ahadi aliyoitoa kwa Jumuiya ya Uchumi ya nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS ya kurejesha utawala wa kiraia katika kipindi cha miaka miwili. Damiba ambaye naye alichukua madaraka kwa njia ya mapinduzi ya kijeshi mwezi Januari, jana amekimbilia kwenye mji mkuu wa Togo, Lome.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents