Burudani

Amini: Nakiheshimu sana kipaji cha mke wangu

Muimbaji na mtunzi wa nyimbo, Amini amedai kuwa sababu za kumshirikisha mke wake Namcy kwenye wimbo wake mpya ni kwakuwa yeye pia ni msanii na anaheshimu kipaji alichomkuta nacho.

Amini

“Unajua huyu sasa hivi ni mke wangu na pia tumepitia mengi sana, raha na matatizo kwahiyo niliamua kuheshimu kipaji chake ambacho nilimkuta nacho ambacho na yeye ni mwanamuziki kama mimi,” Amini ameiambia Bongo5.

“Mwanzo palikuwa na kaugumu kidogo kufanya wote kazi si unajua tena mkiwa studio tofauti na mkiwa nyumbani lakini mambo yakaenda sawa. Pia kuna kazi nyingine itakuja ambayo tuko pamoja,” ameongeza Amini.

“Wimbo ujumbe wake nadhani unajielezea vizuri tu ukisikiliza na hii ni kwa wote ambao wanapendana na wana true love ya ukweli. Na pia nimepata simu kutoka nje ya nchi kama Nigeria pia kuna baadhi ya redio wanaucheza na club na UK.”

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents