Habari

Angekuwa Mwanasiasa: Witness angefuta malipo ya kodi ya nyumba kwa mwaka

Kwa waliopanga, wanajua muziki wa kulipa kodi ya nyumba kwa mwaka. Ni headache hasa ukilinganisha na mishahara au kipato wakipatacho wengi kwa mwezi.

419179_3142633055965_52030459_n

Rapper wa kike nchini, Witness amedai kama angekuwa mwanasiasa, angehakikisha kodi hiyo kandamizi inafutwa kabisa. Lakini wenye nyumba watamuelewa?

“Sipendi siasa (si Hasa) kabisa ila ninatamani siku moja tu ningepewa nafasi ya kuongelea suala la kodi ya nyumba kuwa tunalipa kila mwezi ama miezi mitatu mitatu kama nchi za jirani hapa hapa africa mashariki maana ukiongelea nchi za mbali unaweza onekana unawafyagilia jamani tunaumia mno na kodi za mwaka mzima, na ninajua nina wawakilisha wananchi wengi kila mtu na kodi yake, habari hizi ziwafikie wawakilishi wetu wabunge,” ameandika Witness kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents