Burudani

Angélique Kidjo ambwaga Wizkid tuzo ya Grammy upande wa album bora

Mwimbaji wa Benin Angélique Kidjo na DJ Black Coffee wa Afrika Kusini wameshinda tuzo katika Grammys mwaka huu. Kidjo alishinda albamu bora ya mwaka ya muziki wa dunia kwa ajili ya albamu yake ya Mother Nature. Iliwashirikisha wanamuziki wa Nigeria Burna Boy, Yemi Alade na Mr Eazi.

Mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 61 aliwashinda Wanigeria Wizkid, Femi Kuti na Mghana Rocky Dawuni katika tuzo hiyo.

Huu ulikuwa ushindi wake wa tano wa Grammy baada ya kushinda kitengo hicho mnamo 2014, 2015, na 2019.

Katika hotuba yake ya kukubali tuzo alitoa pongezi kwa wasanii wa kizazi kipya barani Afrika ambao alisema watatamba katika sanaa ya muziki ulimwenguni.

Black Coffee wa Afrika Kusini alishinda albamu bora ya muziki wa densi/kielektroniki. Alishinda tuzo ya albamu yake ya Subconsciously.

Ilikuwa ni tuzo yake ya kwanza kabisa ya Grammy. Alikubali tuzo hiyo pamoja na mwanawe mkubwa, Esona.

“Nataka kumshukuru Mungu kwa zawadi ya muziki na kuweza kuishiriki na ulimwengu na kuponya roho na kusaidia watu kupitia chochote wanachopitia maishani,” alisema.

Ikumbukwe, Wizkid alitajwa kuwania vipengele viwili kwenye tuzo hizo; Best Global Music Perfomance (Essence) na Best Global Music Album (Made In Lagos: Deluxe Edition).

Mwanamama huyo toka Benin ameibuka mshindi wa kipengele cha Best Global Music Album kupitia album yake ‘Mother Nature’ akiwa amemuangusha Wizkid na album yake ‘Made In Lagos: Deluxe Edition’ ambayo ilikuwa inapewa nafasi kubwa ya kushinda.

 

Wizkid pia alibwagwa kwenye kipengele cha Best Global Music Performance, ambacho `#Essence ya Wizkid iliingia katika kinyang’anyiro hicho, imebebwa na Arooj Aftab ambaye ni raia wa Pakistani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents