Burudani

Angélique Kidjo na Black Coffee walioshinda tuzo ya Grammy 2022

Kila mmoja anafahamu kuwa usiku wa kuamkia leo Tuzo kubwa ulimwenguni za Grammy zimetolewa katika jijini Los Angeles nchini Marekani huku wasanii kibao wakiondoka na ushindi.

Katika bara la Afrika wasanii wawili tu ndio walibahatika kushinda tuzo hiyo kubwa kabisa ya Grammy. wasanii hao ni Mkongwe Angélique Kidjo kutoka Benin na DJ maarufu kutoka nchini Afrika Kusini black koffe.

Kidjo alishinda albamu bora ya mwaka ya muziki wa dunia kwa ajili ya albamu yake ya Mother Nature. Iliwashirikisha wanamuziki wa Nigeria Burna Boy, Yemi Alade na Mr Eazi.

Mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 61 aliwashinda Wanigeria Wizkid, Femi Kuti na Mghana Rocky Dawuni katika tuzo hiyo.

Huu ulikuwa ushindi wake wa tano wa Grammy baada ya kushinda kitengo hicho mnamo 2014, 2015, na 2019.

Katika hotuba yake ya kukubali tuzo alitoa pongezi kwa wasanii wa kizazi kipya barani Afrika ambao alisema watatamba katika sanaa ya muziki ulimwenguni.

Black Coffee wa Afrika Kusini alishinda albamu bora ya muziki wa densi/kielektroniki. Alishinda tuzo ya albamu yake ya Subconsciously.

Ilikuwa ni tuzo yake ya kwanza kabisa ya Grammy.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents