Burudani

Asante mke wangu kwa kunifanikisha kuacha bangi, fegi, mirungi na pombe – Mr Blue

Mr Blue byser ametangaza hadharani kuwa sasa sio mfuasi tena wa vilevi vya aina yoyote, na ashukuriwe mke wake kwa kuwezesha hilo.

Mr Blue

Kupitia akaunti yake ya Instagram, hit maker huyo wa ‘Pesa’ amekiri kuwa sasa ana furaha zaidi baada ya kufanikiwa kuacha kuvuta bangi, sigara (fegi) mirungi na pombe. Amemshukuru mama mtoto wake aitwaye Wahyda kwa kumuwezesha kuacha kutumia vilevi hivyo.

Hiki ndicho ameandika Blue:

“Alhamdulilahi ..nimeamka salama nikiwa mwenye furaha ahsante mungu ..na nashukuru pia kwa kufaulu mtihani ahsante mke wangu@wahyda_bysers_heart kwa kunifanikisha kuacha vilevi vyote..(bangi, fegi, mirungi, pombe) na kuishi km binadamu wa kawaida..nawashauri ndugu zangu kuwa makini na marafiki wengine wapo kwa ajili ya kukuharibia maisha yako ..kuwa makini… “

Mr blue

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents