Burudani

Ray C alia kwa uchungu baada ya kunyimwa tiba ya Methadone (Video)

Rehema Chalamila aka Ray C amejikuta akishindwa kujizuia kulia baada ya kunyimwa dawa ya Methadone ambayo amekuwa akiitumia kwa miaka miwili sasa ili kumsaidia kuondokana na addiction ya madawa ya kulevya.

https://youtu.be/iJoIPUvZTuo

Ray C amepost video kwenye Instagram ambazo kwa zinaendelea kusambaa kwenye mtandao huo akilia kwa uchungu.

“Nashindwa kuvumilia,” anasikika akisema. “Mpaka sasa nipo hapa kitengo cha madawa na sijapewa dawa, kwa sababu nilipost ile post nyingine wamenifanyia makusudi. Sasa mimi nikikosa madawa wanataka nirudi kwenye kuvuta unga,” amehoji muimbaji huyo.

Ray C aliendelea kudai kuwa mwili unamuuma pamoja na mifupa huku akishindwa kujua afanye nini ili kukabiliana na hali hiyo ambayo amedai inamtesa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents