Afya

Austria yatangaza Lockdown kwa watu ambao hawajachanjwa

Takriban watu milioni mbili ambao hawajachanjwa kikamilifu dhidi ya Covid-19 wamewekwa chini ya zuio la kutotoka nje nchini Austria huku nchi hiyo ikikabiliwa na kuongezeka kwa visa vya ugonjwa huo .

“Hatuchukui hatua hii kirahisi, lakini kwa bahati mbaya ni muhimu,” Kansela Alexander Schallenberg alisema.

Watu ambao hawajachanjwa wataruhusiwa tu kuondoka nyumbani kwa sababu chache, kama vile kufanya kazi au kununua chakula.

Takriban 65% ya wakazi wa Austria wamechanjwa kikamilifu – mojawapo ya viwango vya chini kabisa Ulaya Magharibi.

Wakati huo huo, kiwango cha maambukizi ya siku saba ni zaidi ya kesi 800 kwa kila watu 100,000, ambayo ni moja ya juu zaidi barani Ulaya.

Kwa ujumla, Ulaya imekuwa tena eneo lililoathiriwa zaidi na janga hili na nchi kadhaa zinaanzisha vizuizi na onyo la kuongezeka kwa visa vya ugonjwa huo

Walakini, Uingereza, ambayo ina moja ya viwango vya juu zaidi vya maambukizi ya Covid, bado haijaleta vizuizi, licha ya viongozi wa afya kutaka sheria kama maski za lazima katika maeneo yaliyo na watu wengi na zilizofungwa zirudishwe ili kuepusha hali mbaya zaidi msimu wa baridi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents