Burudani

Baada ya kujifungua,Travis Scott ampa zawadia nono mpenzi wake

Rapper Travis Scott ameonyesha yeye sio mtu wa mchezo mchezo hasa linapokuja jambo kuhusu mpenzi wake Kylie Jenner kutoka familia ya Kardashian.

Rapper Scott ameona isiwe shida amemtununu mzazi mwenzake huyo ndinga mpya aina ya Ferrari, kama zawadi baada ya kumletea mtoto wa kike aitwaye Storm hivi karibuni.

Gari hiyo aina ya Ferrari yenye rangi nyeusi imekadiriwa kuwa na thamani ya kiasi cha dola milioni 1.2 sawa na kiasi cha shilingi bilioni mbili na ushehe za Kitanzania.(2,697,263,826.90)


Kwa sasa wawili hao wamekuwa wakidandana kila waendapo na picha ya kwanza imenaswa wakiwa katika mtoko wao wa kula chakua cha mchana maeno ya Nobu mjini Malibu, nchini Marekani. Picha za gari hiyo ziliweka katika mtandao wa kijamii wa Instagram wa mrembo huyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents