Burudani

Baada ya kuolewa Meninah asimama kufanya muziki kwa muda!

Baada ya kuolewa muimbaji wa ‘Shaghala Baghala’, Meninah Atick amesema amesimama kufanya muziki kwa muda.

11326182_1693295520903189_1185107284_n

Akizungumza na kipindi cha Friday Night Live cha EATV hivi karibuni, Meninah alisema muda mwingi atautumia kufanya biashara.

“Mimi ni Mrs Abdukarim, alikuwa ana support muziki wangu, but mimi kama mimi kwanza nilikuwa engaged nilikubaliana na hiyo hali na ni kijana mwenzangu pia tunapendana, nikachagua nisimamishe kazi zangu za muziki kwa wakati huu kwa sababu kwanza nilikuwa busy na kusimamia biashara zangu,” alisema.

“Halafu pia kwa sababu nina kampuni yangu ya Meninah Investment Company inayoshughulika na catering, events plan, events management pamoja na vitu vingine vya burudani, so nakuwa busy sana na project zangu ila watu watazidi kunisikia na kuniona Meninah,” aliongeza.

Kwa upande mwingine Meninah alisema hakupenda kuiweka wazi ndoa yake kwakuwa hakutaka aonekana kama ana’show off.’

“Mimi mambo yangu sipendi kushow off,” alisisitiza. “Kama nina lengo na jambo langu, naangalia mbali kwa sababu ukifanya jambo lako la heri lazima ufanye kimya kimya kwanza.”

“Watu walishazoea kuona harusi za mastaa zina presha matangazo kila mtu ajue, ila kwangu mimi hili ni jambo la heri, sikuhitaji kuliweka wazi mapema kabla sijafanikiwa ninachohitaji. Kwahiyo niliamua kufanya kwanza ndoa ili kutia kwanza baraka, halafu reception inakuja.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents