Habari

Baada ya kuwa na watoto 102, wajukuu 568 Mzee Musa asema wanatosha

Mzee Musa Hasahya, mkulima kutoka nchini Uganda mwenye wake 12, watoto 102, na wajukuu 568, ameamua kuacha kuongeza familia ambayo tayari imekuwa kubwa.

Baada ya miaka mingi ya kulea familia hiyo kubwa, mzee huyo mwenye eneo la heka mbili za ardhi amependekeza wake zake waanze kuzingatia udhibiti wa Uzazi wa Mpango kutokana na uhaba wa rasilimali na matatizo ya kifedha.

Musa ambaye watoto wake wengine amewasahau majina, amejitahidi kusomesha baadhi, sasa anaomba usaidizi wa serikali.

Imeandikwa na @fumo255

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents