BurudaniHabari

Tems hajatoka kapa tuzo za Grammy, Burna boy akosa tuzo

Mwimbaji wa Nigeria, Temilade Openiyi, maarufu kama Tems, ameshinda tuzo yake ya kwanza ya Grammy.

Alishinda tuzo hiyo katika hafla inayoendelea kwenye ukumbi wa Crypto.com Arena huko Los Angeles Jumapili.

Mchango wake kwenye wimbo ‘Wait For U’ wa Future akimshirikisha Drake ulimpa tuzo hiyo.

PUNCH ilikuwa imeripoti hapo awali kwamba Tems alikuwa miongoni mwa wageni walioalikwa kwenye hafla ya kila mwaka ya Roc Nation kabla ya Grammy Brunch siku ya Jumamosi.

Katika video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii, Tems, ambaye alivalia gauni jeupe, alionekana akizungumza na mwanzilishi wa Roc Nation Jay-Z na mkewe, Beyoncé.
Tafrija ya kabla ya Grammy ilifanyika katika makazi ya kibinafsi huko Bel-Air, Los Angeles.

Wakati huo huo, mwimbaji aliyeshinda tuzo, Damini Ogbulu, anayejulikana zaidi kama Burna Boy alipoteza uteuzi mara mbili.

Alipoteza kategoria ya ‘Best Global Music Album’ na ‘Best Global Music Performance’.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents