Burudani

Banana Zorro aeleza sababu za kuitia kapuni kwa muda kolabo yake na Young Killer

Banana Zorro amesema ameshindwa kutoa kolabo yake na Young Killer Msodoki iliyofanyika katikati ya mwaka 2015 kwa madai muda wa hadhi ya kazi hiyo bado haujafika.

Banana

Banana ameaimbia Bongo5 kuwa ameona kuitoa kazi hiyo kwa muda huu ni kuiharibu.

“ideo imekamilika na audio yaani kila kitu,” amesema. “Sema timu yangu ambayo nafanya nayo kazi tumekaa na kujadiliana hii ngoma ni kali sana lakini kutokana na soko jinsi lilivyokaa na ushindani uliokuwepo kwa sasa hivi tumeona nyimbo ni nzuri lakini kwa mbele kidogo,” ameeleza.

Ameongeza, “Yaani ngoma jinsi tulivyoifanya ni kwa muda wa mbele kwa sasa tutaipoteza. Ngoma iko sawa na kila kitu kipo sawa, rap kali, muziki na video kali lakini kuanzia idea ya wimbo mpaka video na aina ya muziki tuliopiga ni ngoma kubwa sana. Kwahiyo kwa sababu nilikuwa kimya muda mrefu bila kutoa ngoma, nikasema ngoja nianze na ‘Kasema Tena’ na baada ya hapo tutajua nini kinakuja.”

Kabla ya hapo Young Killer alimshirikisha muimbaji huyo kwenye wimbo wake uitwao Nimebadilika.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents