Habari

Barnaba: Siku ya kurekodi ‘Love Me’ Izzo Bizness na Master Jay walikuwa na wasiwasi kama nitakaa vizuri

Story ya nyuma ya pazia ambayo wengi hawakuifahamu kuhusu wimbo wa Izzo Bizness aliomshirikisha Barnaba na Shaa ‘Love Me’ ni kuwa, mwanzoni producer Master Jay na Izzo mwenywe hawakuwa na imani kama Barnaba atafaa kushirikishwa.

https://youtu.be/Q_a7w8FfG_k

Barnaba amesema kuwa walimuuliza mara mbili mbili kama kweli atakaa vizuri kwenye wimbo huo ambao ulikuja kuwa miongoni mwa ngoma kali za Hip Hop zenye chorus kali zilizotoka mwaka 2013.

“Nashukuru sana kufanya kazi na Izzo Bizness kwani ni moja ya rapper ambaye namkubali na kumheshimu na ninakumbuka nilikuwa na mpango wa kufanya kazi na moja ya rapper hapa nyumbani ila alipotokea Izzo nilishukuru maana nilikuwa natimiza moja ya malengo yangu. Nakumbuka siku ya kufanya wimbo huo Izzo Bussiness pamoja na Master Jay walikuwa na wasiwasi wakidhani labda ningeshindwa kukaa vizuri katika ule mdundo lakini niliwaambia ondoeni shaka maaana mimi ndiyo Barnaba Classic” Barnaba aliiambia EATV.

Aliendelea;

“Wakati nafanya ule wimbo Izzo B aliniuliza mara nyingi sana Barnaba utakaa humu kweli hata producer wetu Master Jay alikuwa hana uhakika na yeye aliniuliza kweli Barnaba unaweza kukaa humu na nilipofanya kitu kizuri kilitokea na kweli ni moja ya wimbo ambao umeniongezea mashabiki sana hasa wale ambao walikuwa hawapendi muziki wangu walianza kunikubali kupitia collabo hiyo. Hivyo namshukuru sana Master Jay, na Shaa ambao wao walimshauri Izzo B nifanye nae wimbo ule pia nashukuru na Izzo B mwenyewe maana tulifanya kitu kizuri na watanzania walikipenda zaidi.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents