Burudani

Ben Pol asifia vipaji vya wasanii wa Bongo

Msanii wa R&B Ben Pol amewasifia wasanii wenzake wa Bongoflava kuwa wana uwezo mkubwa kuliko hata wasanii wa nchi zilizoendelea kama Marekani kwa uwezo wao wa kufanya kazi nyingi zikiwemo utunzi na kuimba wao wenyewe.

Walter na Ben Paul wakiimba pamoja (640x427)

Kupitia Twitter Ben Pol ambaye mwaka jana na mwaka huu amehit na ngoma kama Pete na Yatakwisha amesema, “wasanii wa Bongo tuna vipaji vya hali ya juu, mtu unafanya kila kitu mwenyewe na bado unaweza kutunga na kutoa Hits, hii hata R.kelly hawezi.”

Ameongeza kuwa kutokana na mazingira ya muziki wa kibongo msanii hujisimamia mwenyewe anapotaka kurekodi, kushoot video ama kujiandaa na show ilhali wasanii wakubwa mfano wa Marekani huwa na watu wanaosimamia mambo hayo.

Amesisitiza kuwa msanii hulazimika kufanya kila kitu kwasababu hawezi kumudu kuajiri watu wa kusimamia mambo hayo. “Sasa watu hawataki kulipa vizuri, mwishowe tunashindwa kutoa ajira kwa wenzetu wenye utaalam fulani fulani wa marketing n.k.”

Wasanii wengi wakubwa katika nchi zilizoendelea huandikiwa nyimbo zao (mashairi na melody) na watu maalum (songwriters) ambao hutafutwa na record label husika kwa kazi hiyo na wao huingia tu studio kurekodi tofauti na wasanii wengi wa Tanzania (na kwingineko Afrika) ambao hutunga na kuimba wenyewe.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents