Burudani

Ben Pol azungumzia picha zake za utupu (Video)

Baada ya Ben Pol kuchafua hali ya hewa kutokana na picha zake zinazomuonyesha akiwa mtupu kuenea mitandaoni na kumsababishia kukutana na mvua kubwa ya matusi, msanii huyo amefunguka sababu ya kufanya hivyo.

Akiongea na Bongo5, Ben amesema unapoachia wimbo unatakiwa kuhakikisha maudhui yake yanakuja kufanana na picha zake ili ziweze kuonyesha uhalisia, na ameongeza kuwa wazo la kupiga picha hizo lilitoka kwake na kuushirikisha uongozi wake.

“Muziki au sanaa ni kama bidhaa nyingine, unajua unavyotaka kufanya promotion ya kitu chako unatoa material zote ambazo zinashabiana na ile bidhaa yako, kama wewe una kampuni ya nyumba au viwandaunaweza kutoa vitu vingine ambavyo labda vinarelate na ile bidhaa yako. Mimi nilikuwa natoa nyimbo ambayo project yangu inayofuata maudhui yake ni yakutekwa, unatoa wimbo ambao content yake inazungumzia hali ya kutekwa kwa hiyo materiall zake za kupromote ambazo sisi tunatumia artwork kama wasanii lazima ionyeshe feeling ya kutekwa, lazima ielezee art ambayo mtu hana uhuru, hana haki, hana power, hana privacy, hana faragha hata ya mwili wake, hata mawazo yake, hata simu yake hamna mawasiliano hamna kiti chochote. Kwa hiyo ilikuwa ni lazima material zangu za kupromote projrct yangu ambayo maudhui yake ni kutekwa, zile material zilikuwa lazima ziwe na feeling ya kutekwa,” amesema hitmaker huyo wa Phone.

“Siyo kila mateka lazima ae vila lakini mateka anaweza kuwa vyovyote, unavyochukuliwa uhuru wako, unavyochukuliwa haki zako unavyochukuliwa faragha yako usiri wako, power zako unaweza kufanywa chochote kwa hiyo unaweza kuwa vyovyote, ningeweza kuwa na kipara pale nimenyolewa hata na kisu. Hiyo ndio maana ya nimetekwa huna power, huna sauti, chochote unaweza ukafanyiwa. Kwa hiyo mimi art yangu ilikuwa inaonyesha hali ya kutekwa, hali ya kutekwa ina matokeo yoyote yale huwezi kutegemea nini kitatokea. Hakukuwa na uhusianowo mambo yanayoendelea na wazo langu mimi, mimi nimeutunga ule wimbo, nimeurekodi nikawaza huu wimbo ninazungumzia kutekwa, nimetekwa kiasi kwamba sijui kinachoendelea kwenye mji wangu, kwenye nchi yangu,” ameongeza.

“Wazazi wamenipigia simu na baba yangu ananipigia simu karibia kila siku, tangu yale mambo yameanza ananipigia simu sio chini ya mara mbili kwa siku. Mwanzo walishtuka sana, waliogopa, walikuwa confused kwamba umetekwa na umefungwa kamba uko wapi? Whats going on? Wazazi wangu hawapendagi kuwa to negative na wakiangalia zile picha umefungwaq kama unateswa. Uko wapi? Nini kinaendelea? Hilo ndio swali la kwanza mzee amenipigia, kwa hiyo waliogopa hivyo, mama yangu pia alishtuka baadae akaangalia akaona kama na yeye pia inamuumiza, inamtesa, ameshindwa kulala Ijumaa. Akijaribu kupekuwa huku na kule watu wanaongelea halafu mimi siongelei, sionekani popote nikiongea ikawa inamuumiza, akawa anampigia mdogo wangu, yuko wapi jamaa na nini kinaendelea?,” amesisitiza.

Kwa sasa muimbaji huyo ameachia wimbo wake mpya uitwao ‘Tatu’ amabo amemshirikisha rapper Darassa huku baadhi ya picha hizo zilizoonekana kuzua utata zikitumika katika kutengenezea cover z wimbo huo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents