Burudani

Ben Pol aizungumzia hatua ya Diamond kumsaini Rich Mavoko katika label yake ya WCB

Mkali wa wimbo ‘Moyo Mashine’, Ben Pol amefunguka na kuzungumzia hatua ya Diamond Platnumz kumsani msanii mkubwa kama Rich Mavoko katika label yake WCB.
ben paulo

Akiongea na Bongo5 hivi karibuni, Ben Pol amesema hatua ya Diamond kuamua kumsaini Rich Mavoko katika label ya WCB, itafungua njia kwa wasanii wengine kuwa na moyo wa kusaidiana wenyewe kwa wenyewe.

“Ni vizuri sisi kwa sisi tukaaminiana na kufanya kolabo kwenye kazi,” alisema Ben Pol. “Diamond ni mpiganaji na Mavoko ni mtu ambaye ana kipaji na mjanja mjanja, kwahiyo muungano wao unaweza kuleta mapinduzi makubwa katika muziki.”

Pia muimbaji huyo amewataka wale wasanii wenye uwezo wa kuwasaidia wenzao wasisite, kwani hiyo ndiyo njia sahihi ya kuupeleka muziki wa Tanzania mbele zaidi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents