HabariSiasa

Biden, Xi kuzungumza 

Rais Joe Biden anatarajiwa kuzungumza kwa njia ya simu na kiongozi wa China Xi Jinping  Alhamisi.

Duru inayofahamu mipango hiyo inasema mazungumzo hayo yatafanyika wakati ambapo kuna mivutano mipya kuhusu Taiwana na Urusi kuivamia Ukraine.

Msemaji wa usalama wa ikulu ya White House John Kirby amewaambia waandishi wa habari kwamba suala la ushindani wa kiuchumi kati ya nchi hizo mbili pia ni suala litakalojadiliwa na viongozi hao katika mazungumzo hayo.

Hii itakuwa mara ya tano ambapo viongozi hao wawili wanazungumza kwa njia ya simu. China imetoa onyo kwa serikali ya Biden kuhusiana na spika wa bunge Nancy Pelosi kufanya ziara Taiwan, kwani China inasema hilo ni eneo lake. Marekani nayo imesema haiondoi uwezekano kwamba China inaweza kumshambulia Pelosi endapo atafanya ziara hiyo.

Related Articles

Back to top button