Burudani

Billnass aeleza wakati wake mgumu katika muziki

Msanii wa muziki wa Hip Hop, Billnass amefunguka kwa kudai kuwa siku mbaya katika maisha yake ya muziki ni siku ambayo anaachia wimbo mpya.

Rapa huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Mazoea’ akiwa amemshirikisha Mwana FA, ameiambia Bongo5 kuwa siku hiyo huwa na wasiwasi juu ya kile anachokipeleka kwa mashabiki wake.

“Siku ambayo huwa inanisumbua ni siku ambayo naachia wimbo mpya na ni siku moja tu,” alisema Billnass. “Huwa nakuwa na wasiwasi kuhusu kazi yangu mpya lakini baada ya muda tu hali inabadilika na pia hali hii inanikuta katika nyimbo zangu nyingi,”

Rapa huyo ambaye pia ni mwanafunzi wa Chuo cha Uhasibu Posta, amewataka mashabiki wa muziki wake kukaa mkao wa kula kwaajili ya ujio wa kazi zake mpya.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents