Habari

Marekani yafunga mtambo wa kuilinda Korea Kusini dhidi ya Korea Kaskazini

Korea Kusini imesema wanajeshi wa Marekani wameanza kujenga mitambo wa kisasa wa kuzuia makombora katika eneo moja kusini mwa nchi hiyo.


Picha ya mtambo huyo jinsi unavyofanya kazi ya kuzuia makombora

Mtambo huo wa kujilinda dhidi ya makombora,ambao hufahamika kitaalamu kama THAAD, kwa Kiingereza, ‘Terminal High Altitude Area Defense’,kutokana na wasiwasi wa tishio kutoka kwa Korea Kaskazini ambayo imeendelea kufanyia majaribio makombora.

Wizara ya ulinzi ya Korea Kusini imesema mtambo huo utakamilishwa na utakuwa tayari kutumika katika kipindi cha mwaka mmoja.

Kumekuwepo na taarifa za kutokea kwa makabiliano kati ya wenyeji na polisi eneo panapojengwa mtambo huo, ambalo awali lilikuwa uwanja wa mchezo wa gofu.

Mtambo huo unajengwa katika wilaya ya Seongju.

China imekuwa ikipinga kuwekwa kwa mtambo huo.

Rais wa Marekani Donald Trump ameashiria kwamba Marekani iko tayari kuchukua hatua kivyake bila kuishirikisha China kukabiliana na tishio la nyuklia kutoka kwa Korea Kaskazini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents