Burudani

Game halijakaa poa, so sitoi muziki muda huu – H.Baba

H Baba amefunguka sababu ya kushindwa kuachia ngoma mpya kwa muda mrefu.

Japo muimbaji huyo tayari ameshafanya baadhi ya kolabo na wasanii kutoka nje ikiwemo wa nchi za Congo DRC, amesema hawezi kuziachia kwa sasa kwa kuwa muda wake wa kufanya hivyo haujafika.

“Natoa wimbo kulingana na game linavyokwenda, game halijakaa poa sasa hivi so siwezi kutoa wimbo. Sababu haitakuwa kitu kizuri kulingana na wakati. Nitatoa wimbo leo na kesho utazimwa nitafaidika nini? Mimi gharama zangu za kwenda Kinshasa huko nimegharamikia matiketi ya ndege na hoteli na kila kitu zije kuishia hewani? Sifanyi hivyo natafuta muda wangu mzuri wa kuachia ngoma,” amesema H Baba.

Msanii huyo ameongeza kuwa,katika muziki wake hataki kuwa na menejimenti masikini kwa kuwa asilimia yao kubwa wanategemea msanii afanye kazi ndio na wao wale.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents