Habari

Halima Mdee aomba msamaha kwa Spika na Dr Kigwangalla.

Mbunge wa Kawe, Halima Mdee alisimama mbele ya bunge na kuomba msamaha ikiwa ni wiki kadhaa tangu atuhumiwe kosa la kutumia lugha cha chafu kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai.

“Mwenyekiti tarehe nne mwezi wa nne wakati wa uchaguzi wa Iyala kuna matuklio ambayo yalitokea yakanipelekea kuzungumza lugha ambayo kitamaduni za Bunge sio sawa na lugha husika ilimgusa muheshimiwa spika na muheshimiwa Kigwangalla kwa namna moja au nyingine kama mbunge mzoefu nilitumia kuzungumza na kuomba radhi wahusika katika individual capacity lakini vilevile nikaona ni busara kwasababu haya maneno nilizungumza bungeni lakini pia kuzungumza na kumuomba radhi Muheshimiwa Spika kwahiyo niliomba huu muda specifically kumuomba radhi kumuambia namheshimu na kumwambia sitarudia, spika ni kiongozi wangu lakini pia ni mwananchi wa jimbo la Kawe,” aliomba radhi Mdee.

“Kwahiyo nina kila sababu yakuyazingatia haya mawili kwa umakini mkubwa kwahiyo ninaomba radhi kwake ninaomba radhi kwa Kigwangalla ninaomba radhi wka Bunge, ninaomba radhi kwa wananchi wa bunge la Kawe ambao miongoni mwenu nyie ni miongoni mwa wananchi wa jimbo la Kawe na niwaaahidi tu kuna baadhi ya wananchi Watanzania ntakuwa nimewakawanza kwahiyo ninaomba radhi niaahidi tu michango yangu ya bunge itaendelea kama kawaida lakini kwa kutumia lugha za staha.”

Mbunge huyo alitoa lugha za matusi kwa Spika wakati wa uchaguzi wa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki uliofanyika April 4, 2017.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents