Habari

Picha: Rais Magufuli awasili rasmi katika sherehe ya miaka 53 ya Muungano

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli, amewasili rasmi katika maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, yanayofanyika kitaifa katika viwanja vya Jamhuri mjini Dodoma.

Sherehe hizo hupambwa na maonyesho mbali mbali ya kijeshi na gwaride mbalimbali ambapo tayari vikosi mbalimbali vinaendelea kuonyesha maonyesho yake uwanjani hapo.



picha na Ikulu

Uwanja huo umepambwa kwa rangi ya bendera ya Tanzania na Viongozi mbalimbali wa Kiserikali wameshawahi uwanjani hapo kwaajili ya kusherehekea sherehe hiyo akiwemo Rais wa Zanzibar, Dkt Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais Bi Samia Suluhu, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents