Burudani

Bongo hakuna msanii anayeweza kufanya trap vizuri – Chin Bees

Msanii wa Bongo Flava, Chin Bees ameeleza sababu ya kufanya muziki aina ya trap.

Chin Bees ambaye anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Kababaye’ ameiambia XXL ya Clouds Fm kuwa anafanya trap kwa sababu Bongo hamna msanii anayefanya muziki huo vizuri.

“Nafanya kutokana naona Bongo hakuna msanii anayeweza kufanya trap vizuri, wanafanya tu kwa sababu ya beat lakini kuna technique zake inabidi uzifuate,” amesema Chin Bees

“Off course wapo watu wanafanya trap lakini naona kama mimi nafanya better sana, still pia namshukuru Mungu ngoma zangu nakuwa siandiki lakini nakuwa nafanya zinakuwa kubwa,” ameongeza.

Ametaja ngoma ambazo alitoa bila hata kuandika ni kama Pepeta, Zuzu na Kababaye.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents