Michezo

Brazil ya Neymar yainyoosha Argentina ya Messi

Timu ya soka ya wanaume ya Brazil ya Neymar, imefanikiwa kuifunga timu ya Argentina ya Messi mabao 3-0 kwenye mchezo wa kufuzu kucheza kombe la dunia nchini Urusi mwaka 2018.

mmg_4106

Mchezo huo ulifanyika kwenye uwanja wa Belo Horizonte, Brazil na wenyeji kufanikiwa kuibuka na mabao hayo kupitia kwa wachezaji wake Philippe Coutinho aliyefunga goli la kwanza kwenye dakika ya 25, Neymar aliyefunga dakika ya 45 na goli la mwisho lilifungwa dakika ya 59 na Paulinho.

Ushindi huo umeifanya timu hiyo ya Brazil kuongoza kundi la timu za bara la Amerika ya Kusini ikiwa na pointi 24 kati ya michezo 11 waliocheza mpaka sasa huku Argentina ikibakia kwenye nafasi yake ya sita ikiwa na pointi 16.

Matokeo mengine ya michezo ya kuwania kufuzu kombe la dunia iliyochezwa alfajiri hii kwenye bara hilo ni:

Uruguay 2 – 1 Ecuador
Paraguay 1 – 4 Peru
Venezuela 5 – 0 Bolivia
Colombia 0 – 0 Chile

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents