Habari

Mbunge wa Zanzibar (CCM), Hafidh Ali Tahir amefariki dunia

Mbunge wa Jimbo la Dimani Zanzibar (CCM), Hafidh Ali Tahir amefariki dunia alfajiri ya kuamkia leo katika Hospitali ya mkoa wa Dodoma.
????????????????????????????????????
Katibu wa Bunge Dk Thomas Kashilila ameliambia gazeti la Habarileo asubuhi hii kuwa Tahir alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya moyo japo si kwa kiwango kikubwa na alikuwa akipata matibabu na kuebndelea na shughuli zake lakini jana majira ya saa 8 usiku alizidiwa na kupelekwa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma na baadae saa 9 alfajiri ya kuamkia leo alifikwa na umauti.

Dk Kashilila alisema hadi jana jioni alikuwepo Bungeni.

Marehemu alizaliwa Oktoba 30, 1953 na aliwahi kuwa Mkuu wa Sauti ya Tanzania Zanzibar (1970-1978) na amekuwa mbunge tangu 2005 hadi mauti yanamkuta.

Marehemu pia alikuwa mwamuzi wa FIFA na mwana-Yanga kindakindaki na ni jana tu amechaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Tawi la wabunge wanaYanga mjini Dodoma chini ya Uenyekiti wa Venance Mwamoto.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents