Burudani
Lil Wayne aingia studio kuandaa ngoma na Scott Storch
Lil Wayne ameungana na producer wake wa zamani, Scott Storch kuandaa ngoma mpya.
Ni Storch ndiye aliyetoa taarifa za kukutana tena na Weezy kupitia Instagram. “Election is over and storch is at least here to make hits,” aliandika.
Producer huyo na Lil Wayne wamewahi kutengeneza hits pamoja zikiwemo ngoma ya Chris Brown, Gimme That (Remix) na ile ya Fat Joe, Make It Rain.
Kwa sasa Wayne anasubiriwa kwa hamu na album yake, Tha Carter V.