Michezo

Yanga wamaliza mzunguko wa kwanza kwa kuichapa Ruvu Shooting

Klabu ya Yanga ambao ni mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Tanzania bara, wamemaliza michezo ya mzunguko wa kwanza kwa ushindi dhidi ya Ruvu Shooting.

_92389799_img-20161111-wa0000-1

Yanga walipata ushindi wa mabao 2-1 katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa uhuru Jijini Dar es Salaam.

Ruvu Shooting ndio walianza kuzifumani nyavu za Yanga kwa bao la Abdulrahman Mussa kwenye dakika ya saba ya mchezo.

Winga wa Yanga Simon Msuva akaisawazishia timu yake bao hilo kwenye dakika ya 32, kabla ya Haruna Niyonzima kufunga goli la pili na la ushindi katika dakika ya 56 kipindi cha pili.

Yanga wanasalia katika nafasi ya pili wakiwa na alama 33, huku wapinzani wao Simba wakiwa kileleni kwa alama 35.
Ligi kuu inasimama kwa muda na mzunguko wa pili unatarajiwa kuanza kutimua vumbi mwezi Desemba, mwaka huu.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents