Burudani

Bright amtolea povu Baraka The Prince

Msanii wa muziki Bongo Bright , amemjia juu Baraka The Prince kwa kudai kuwa anamuandikia nyimbo.

Bright ameeleza kuwa ana uwezo wa kuandika nyimbo na si kweli kwamba Baraka anamwandikia nyimbo.

“Kiufupi mimi sina madhaifu hayo toka nimeanza muziki A-Z ninafanya mwenyewe, kwanza nyimbo za Baraka zote zina copy right sasa mtu unawezaje kuchukua nyimbo zake.” amesema Brith akupitia ENewz ya EATV.

Mkali huyo wa Nitunzie ameongeza kuwa “Baraka anarudia maneo hata ukisikiliza ngoma yangu ya ‘Nitunzie’ amerudia neno moyo kama mara saba hivi,”

Pia msanii huyo ameeleza kuwa alimpa beat ya ‘Nitunize’ Baraka karibu siku nne , na anashangaa amerudia maneno katika nyimbo hiyo, Bright pia ameshangazwa na msanii huyo anayemiliki ‘BANA’ kurudia maneno ata kolabo zake nyingine kama ya Timbulo.

Bright pia ameeleza kuwa ana uwezo wa kumbadilisha Baraka katika muziki kutokana na kuwa na stoo ya muziki.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents