Diamond Platnumz

#BringBackOurWema:Mashabiki wa Wema wanzisha kampeni dhidi ya Diamond wakidai anamharibia maisha

Kundi la watu wanaojiita mashabiki wa Wema Sepetu, limeanzisha kampeni kwenye mtandao wa Instagram iitwayo #BringBackOurWema likimshinikiza mpenzi wake Diamond Platnumz amrudishe kwenye maisha yake ya zamani na kukuza career yake ya filamu.

Wema akiwa pembeni kumsupport Diamond

Mashabiki hao wanaamini kuwa Diamond anampoteza Wema na amekuwa akitumia umaarufu wake (Wema) kujidhatiti zaidi yeye huku Miss Tanzania huyo wa zamani akiendelea kudidimia.

Hivi ndivyo maelezo yanavyosema:

@diamondplatnumz mambo vipi? Sisi mashabiki wa @wemasepetu tunakuomba umsaidie Wema kama yeye anavyokusaidia. Labda niseme kwa uwazi bila woga kwamba mahali ulipo kimziki umefika sababu ya Wema. Wengine hatukuwa mashabiki wako lkn sababu ya mapenzi kwa Wema tukajilazimisha kukupenda tu… so unajua vema bila wema we mziki huna!

Tunakuteteaga tu lkn huwezi kujilinganisha na wanamuziki wengine tunaowajua wanafanya vema kuliko wewe….leo sitawataja majina! nije kwa point yangu sasa wewe si mwanaume? Tuoneshe sasa! “Umetembea tembea nchi mbalimbali” umekutana na watu wa aina mbali, hujamtambulisha wema huko kibiashara, unaishia kusema maneno maneno ya sifa lkn unamwacha Wema anapotea.

Angekuwa Wema she’s always proud of you kukutaja popote hata angepata ile nafasi ya kuongea na Karuache angekutaja, umeonana na kina Davido+Iyayna bila kutaja waigizaji wakubwa Nigeria…Wema ni brand tunamlinganisha na top stars Africa!! We una nafasi kubwa sana kumfanya Wema aonekane..but what your doing unampoteza kwa makusudi. Unamchezesha viduku, Ulipomwacha alikuwa na maendeleo makubwa alikua ameshatengeneza wanamuziki wake, nyumba yake, kipindi chake cha in my shoes kilianza bila mkono wako. Ukaona hapa atakuzidi na unajua jinsi anavokupenda ukamtumi, hujawahi kusema hadharan feelings zako kwake zaidi ya mafumbo mafumbo
Hujawahi kukanusha ile interview ya spora uliyomdiss vibaya Wema….

Je tueleweje sasa? Si lazima kuanika kila kitu mambo yenu binafsi. Wema haoni kwa sasa sababu ya mapenzi yake kwako…tunakuambia leo kama hauna nia nzuri na Wema tunakuomba umuache. Maana unajua tu akimpigia promo mwanamuziki wake Mirror utapotea kwa game. She has all this power tunaomba usimtumie kwa maslahi yako binafsi. #bringbackourwema.

Haya ni maoni ya wengine:

lula_marii

Daaaaaaah kwa ukweliii wema unalegealegea ..yaani how comes you don’t have any respect from da guy who claims to love yuh?anawezaje kushikashika na kusugulia madem haswaaa ukiwa na yy kwa stage…juzi fiesta everyone saw wat diamond did with linah…wit out even thinking of da feelings of our madam…booooo pliz dnt say that is his professionals…coz its only singing that is his profsional…[email protected] ur eyes….@diamondplatnumz pliiiiiz wit all due respect ,achaaa tabia za utoto

bintijasho

Siku nyingi nilikua nataka kusema hichi kitu lakini leo @mrekebishatabia umesemakweli kabisa @diamondplatnumz anaakili san amepinga hesabu akaona wema anamsanii wake nawema anamashabiki wengi alijua tu mirror atakuja kua juu sasa akaona heri arudia na wema apate kumvuringia mipango yake wallah na muonea huru huyu mdogowangu maski yana siku hizi hata mirror simsikii akimtaja @mrekebishatabia umefanya jambo zuri sana l hope @wemasepetu ataupata ujumbe wako

gennomaxmillan

@diamondplatnumz ww sio mwanammebora kwa wema bali n kvuli cha mwanamme japo mm n nwananch wa kawaida sio star lkn bby wangu kanpa maisha mazur na tunafamilia yenyefuraha.@mekebishatabia maisha ya wema hayavutii kbsa haelewek na ni kwel kbsa biła wema huyo jamaa alkuwa hajui ata kuomba maji kwa kizungu chek wema kajitoa kampa darasa badała alipe fazla anakaz ya kujtangaza na kutukandamizia mdogowetu@wemasepetu mm nakapenda sana kawema ni kazr lkn huwa hakubali ukwel ebu kataa kuanikwa kwa magazet ish kama wakna monalisa jack happy magese nancy angel damas na wengne weng ambao walpata kujulkana kama ww mbona maisha yataenda tu humuon mama krsh alivyo sasa eti mpnz ebu tazama alipo uwoya ameona bora kuish kawaida na bado yupo vzr sana huwez jua kama n mama wa jembe@uwoya kaa na .mwenzako bby anapotea

Katika kile kinachoonekana ni kuwa ni jibu kwa kampeni hiyo, Wema ameandika:

My life my rules!!… !!Unataka kushindana na mimi….? Nakuonea huruma… Wema will always be Wema…!!! I tell you…! Watakucheka watu…

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents