Habari

CAG Assad aliondolewa kinyume cha Katiba- Mahakama Kuu

MAHAKAMA Kuu Masjala Kuu imetamka kwamba kuondolewa kwa aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Assad kulifanyika kinyume cha Katiba.

Jopo la majaji hao lilisema kwamba uamuzi huo umefikiwa baada ya kupitia hoja za pande zote mbili na kubaini kulikuwa na ukiukaji wa Katiba katika kuondolewa kwa mlalamikiwa wa nne (Prof. Assad) katika Ofisi ya CAG kwa mujibu wa kifungu cha 6(1) cha Sheria ya Ukaguzi wa Umma kabla ya kufikisha umri wa miaka 65.

“Kumwondoa mlalamikiwa wa nne katika nafasi yake kunakiuka ibara ya 144(1) ya Katiba,” ilisema sehemu ya hukumu hiyo huku Mahakama ikisema haitoi agizo lolote kuhusu gharama kama ombi lilivyokuwa.

Zitto aliwasilisha maombi dhidi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Charles Kichere (CAG) na Prof. Assad aliyeondolewa madarakani Novemba 2, 2019.

Muda mfupi baada ya kutolewa kwa uamuzi huo jana, Zitto kupitia taarifa yake kwa umma, alisema amefarijika kwa uamuzi huo wa Mahakama Kuu kuhusu shauri hilo.

Hata hivyo, Zitto alisema mahakama imekataa kukubali maombi yao ya kwamba kuteuliwa CAG mwingine ilikuwa batili.

Related Articles

Back to top button