Habari

CCM yavigaragaza vyama vya upinzani kwenye uchaguzi mdogo wa madiwani

Matokeo ya uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata 43 uliofanyika jana Jumapili yanaonesha kuwa CCM imeongoza dhidi ya vyama vya upinzani katika kata mbalimbali baada ya wagombea wake kushinda.

Katika Kata  ya Majengo wilayani Korogwe  mkoani Tanga, Mustapha Shengwatu (CCM) alishinda kwa kura 527 na kuwashinda Abdallah Maonga(Chadema) aliyepata kura 385, Abbas Chomboko (ADC ) kura 17 na Kassim Msenga (CUF) kura 26, ambapo kula halali zilizopigwa ni 955 na zilizoharibika ni 3.

Matokeo ya Kata  ya Mamba wilayani  Lushoto  mkoani Tanga, Richard Msumari(CCM) ameshinda kwa kura  1,399 akiwashinda Jafari Ndege(Chadema) kura  774  na  Nurdini Kipingu(CUF) kura  30.

Katika Kata ya Bomambuzi mkoani Kilimanjaro, Juma Raibu (CCM) ameshinda kwa kura 2,854, Hedlack Minde (Chadema) 1,992, Salim, Mchomvu ( CUF) 17, Issack Kireti( Sau) 00 na Reuben Msuya (UDP)  02

Kata ya Machame Magharibi, Martin Munisi (CCM) kura 1,048 na Bariki Lema(Chadema) 595,

Kata ya Mnadani, Nasibu Mndeme(CCM) 1,708, Ezra Nyari( Chadema) 958, Msafiri Hamisi (ACT-Wazalendo)  14 na Maynard Shoo(NCCR-Mageuzi) 3.

SOMA NA HII – ACT Wazalendo wapoteza kata 17, Waahidi kufanya makubwa uchaguzi wa Wabunge

Kata ya Weruweru, Swalehe Msengesi (CCM) 1,410, Moses Kalaghe (Chadema) 706, Haji Ndarai (CUF) 26, Mabranda Msabaha(ACT-Wazalendo) 3 na Friman Massawe (NCCR-Mageuzi) 00.

Katika Mkoa wa Arusha CCM imefanikiwa kuchukua kata zote tano baada ya Chadema kutangaza kujitoa katika kinyang’anyiro cha uchaguzi huo mapema jana .

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents