Habari

CCM yawanasa wengine watatu toka CHADEMA

Aliyekua mgombea wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA Jimbo la Mvomero mwaka 2015, Mchungaji wa kanisa la Assemblies of God, Oswald Mlay na wenzake wawili wameamua kurejea chama cha mapinduzi (CCM) kwa kile walichodai kuridhishwa na kasi ya utendaji kazi wa Rais Dkt. John Magufuli.

11

Akizungumza na katibu wa mkoa wa chama cha mapinduzi mkoa, Kulwa Milonge, Mchungaji huyo amesema kuwa kwa ridhaa yake mwenyewe ameamua kurejea chama cha mapinduzi kwa kuwa kina sera nzuri na zinazotekelezeka.

“Ninawashukuru kwa kunipokea, mimi ni mfanyakazi nakipenda chama na nina nguvu na ntashilikiana na wananchi wenzangu wa chama cha mapinduzi. Kwakweli niseme Rais Magufuli anafanya kile nilichokuwa nakitaka vile nilivyokuwa navitaka amevifanya na vimeshapitiliza. Kwahiyo sina sababu ya kuwa mnafki kuwa mpinzani na kumuacha mtu kama Rais Magufuli awe peke yake. Kwahiyo narudi nyumbani naomba mnipokee. Katibu ntafanya kazi popote utakapoona nafaa kwa mawazo ushauri kwaajili ya chama chetu,” alisema Mlay.

Wengine waliohamia CCM ni Paul Mboji na Patrick Ambi

Hivi karibuni, Mbunge wa zamani wa NCCR Mageuzi, Moses Joseph Machali alihamia CCM huku naye akidai kuridhishwa na utendaji kazi wa Rais Magufuli.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents