Habari

Polisi ajiua kwa risasi bila kukusudia

Askari polisi mwenye cheo cha Koplo, Evarist Furaha wa Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani amekufa kwa kujipiga risasi kwa bahati mbaya wakati akielekea kwenye lindo kwa Mkuu wa Wilaya ya Kibaha.
3784264_orig

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Blasius Chatanda ameyasema hayo jana kwa waandishi wa habari alipokuwa akitolea ufafanuzi tukio hilo.

Chatanda amesema ajali hiyo ilitokea Novemba 28, mwaka huu saa moja usiku, Maili Moja eneo la Sokoni, Kata ya Maili Mmoja.

“Askari huyo alijipiga risasi kwa bahati mbaya ambapo alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Tumbi,” amesema Chatanda.

Amesema, Furaha aliingia kazini jioni katika Kituo cha Polisi Wilaya ya Kibaha na alikuwa amepangiwa lindo kwa Mkuu wa Wilaya ya Kibaha.

“Alikutwa na mauti baada ya kujipiga risasi kwa bunduki aina ya SMG akiwa anakwenda kwenye lindo alilopangiwa,” amesema na kuongeza kuwa alikuwa anaenda lindoni akiwa amekaa mbele ya gari PT1732 lililokuwa likiendeshwa na Koplo Grayson, ndipo wakati anashuka bunduki ilijifyatua na kumpiga kifuani upande wa kushoto.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents