Burudani

Chaba aeleza kwanini album yake inaitwa ‘Tanzanite Milele’

Rapper wa Arusha, Chaba, ameachia album yake mpya iliyopewa jina, Tanzania Milele.

Alifanya uzinduzi mkubwa wa album hiyo mwishoni mwa wiki jijini humo.

“Jina Tanzanite Milele ni la kisanaa,” ameiambia Bongo5. “Mimi ni madini adimu kama Tanzanite na mistari iliyomo humo ndani ni Tanzanite milele,” amefafanua.

Chaba amewataja wasanii aliowashirikisha kwenye album hiyo kuwa ni pamoja na Vicklicious, Nakaaya, Julie Sanders, J Deal, Hisia, Dx, Chindo man, Nikki Mbishi,Pinda Bway na G Nako.

Pamoja na CD za kawaida, album hiyo pia inapatikana kwenye mtandao Mkito. Bonyeza hapa kuipakua.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents