Siasa

Chama cha Republican chanyakua baraza la Senate, Obama kupunguziwa makali!

Chama cha Republican cha nchini Marekani, kimelinyakua baraza la Senate kutoka chama cha Democratic na hivyo kukipa udhibiti wa bunge la Congress na nafasi ya kumpa wakati mgumu Rais Barack Obama katika miaka yake miwili aliyobakiza ikulu.

_78766643_024602605-1

Chama hicho kimeshinda kwenye majimbo ya Arkansas, Colorado, Iowa, Montana, North Carolina, South Dakota na West Virginia. Katika matokeo hayo ya uchaguzi wa katikati ya muhula, pia kinatarajiwa kuchukua majimbo mengi wakati kura zikiendelea kuhesabiwa.

Chama hicho sasa kinashikilia viti 52 na kinaonekana kitashinda vingine.

Pamoja na kuchukua Senate, Republicans wanaonekana kuongeza nguvu yao kwenye House of Representatives katika kiwango ambacho hakijawahi kuonekana tangu vita vikuu vya pili vya dunia.

Pindi bunge jipya la Congress litakapoapishwa January mwakani, itakuwa ni mara ya kwanza Republicans kushikilia sehemu zote mbili (Senate na House of Representatives) tangu mwaka 2006.

Watakuwa na uwezo wa kupinga agenda nyingi za Obama katika uongozi wake uliosalia.

Kuchukua udhibiti wa Senate utawafanya Republicans wazuie uwezo wake wa kuteua majaji, wajumbe wa baraza na maafisa wa juu wa serikali.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents