Habari

Changamoto ukusanyaji mdogo wa mapato (+Video)

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,(TAMISEMI) Mh. Ummy Mwalimu amemuagiza Mkuu wa Mkoa mpya wa Tabora Dkt Batilda S. Buriani akasimamie vyema kuongeza kiwango cha ukusanyaji wa mapato katika Halmashauri za Mkoa huo ikiwa ni maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hasaan.

Waziri Ummy ameyasema hayo katika hafla ya kuwaapisha Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa ,Ikulu Chawino Jijini Dodoma leo June 21,2021.

Waziri Ummy amesema kuwa mpaka kufikia Mei mwaka huu Mkoa wa Tabora umekusanya asilimia sitini na tisa pekee (69%) huku kitaifa ikiwa ni 94%,hali inayopelekea Halmashauri hizo kupeleka fedha kidogo sana kwenye kutatua kero za Wananchi.

By- BAKARI WAZIRI

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents